Wamarakwet

Wamarakwet ni jina lililobadilishwa kutoka Markweta. Ni kabila dogo katika kabila kuu la Wakalenjin: idadi yao ikikadiriwa kuwa 200,000. Inajumuisha makabila madogo ya Almoo, Cherangany (Sengwer au Kimaala), Endoow, Markweta (kabila dogo linalolipa jina lake la kawaida), Sombirir (Borokot) na Kiptaani ambao wanaishi kwa wingi katika kaunti ya Elgeyo-Marakwet eneo la Kaskazini mwa Bonde la Ufa nchini Kenya. Wengine wao wanaishi katika kaunti za Trans Nzoia Mashariki na Uasin Gishu Kaskazini na miji mingine nchini Kenya. Wachache wamekwenda kuishi katika maeneo ya mbali kama vile Afrika Kusini, Australia na hata Tennessee / Washington / New York nchini Marekani.

Sehemu inayokaliwa na Wamarakwet ndiyo mojawapo wa sehemu za kupendeza sana na maumbile mazuri nchini Kenya, ikipakana kwa sehemu ya mashariki Mto Kerio ukiwa mita 1000 juu ya usawa wa bahari, unaopitia katika sehemu ndogo ya Bonde la Ufa. Katika sehemu ya magharibi, inajumuisha sehemu yote ya milima ya Cherang’any ambayo urefu wake ni mita 3 300 juu ya usawa wa bahari magharibi mwa sehemu ya vilima ya Marakwet.

Makau makuu ya iliyokuwa Wilaya ya Marakwet ilikuwa katika mji ulio kwenye mlima wa Kapsowar. Sehemu nyingine za soko/miji ni Chebiemit, Kapcherop, Cheptongei, Arroor, Chesongoch, Chesoi, Kapyego, Tot, Sangach na Embobut Mosop.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search